RISALA YA ALLAH: “MJA WANGU ATAKUWA HURU KATIKA HESABU (QIYAMA) IWAPO ATATIMIZA SHERIA ZANGU.”
27 Novemba 2023
Bismillahirrahmanirrahiim.
Mja atakuwa huru katika hesabu ya Kiyama ikiwa atatimiza Sheria Zangu, ambazo ni:
Kuto nishirikisha Mimi (Allah) na chochote,
Kutofanya uharibifu katika ardhi,
Kutojiepusha na yale niliyoyaamuru,
Kuwa na huruma kati ya wenzao,
Kutochukua muziki kama mshirika (mwenye kushirikiana na moyo au ibada),
Kutambua kuwa Mimi peke Yangu ndiye niletaye msaada,
Kutojihusisha na wivu (hasad), fitina, au kuchochea ugomvi baina ya watu,
Kujiona kama mja mtiifu kwa amri Zangu na makatazo Yangu,
Kutoogopa wanadamu, bali kuniogopa Mimi pekee,
Kutoamini kuwa binadamu anaweza kuleta kheri au shari; ni Mimi tu Ninaleta mema na mabaya – yaliyojiri au yajayo,
Kutofanya uharibifu kwa wenzao kwa sababu ya fitina,
Kujiepusha kabisa na kila aina ya Shirk,
Na kunikumbuka Mimi kila wakati – Nami Nitamuongoza.
Bismillahirrahmanirrahiim
"Ulaa'ika ‘alaa hudamirrabbihim wa ulaa'ika humul- muflihuun.
"Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu."
Ameen, Yaa Allah, Yaa Rabb, Yaa Sami, Yaa Baswir, Alhamdulillah.
Maneno muhimu:
#Risala ya Ar-Rahman; #Ahmad-Habibi; #Ruqhoyya binti Muhammad; #Mipaka ya Wakati; #Kundi la Upande wa Kulia; #313; #Kundi la upande wa kushoto